Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

JW Library kwa Ajili ya Vifaa vya Windows

JW Library kwa Ajili ya Vifaa vya Windows

JW Library ni programu rasmi iliyotayarishwa na Mashahidi wa Yehova. Inatia ndani tafsiri kadhaa za Biblia, pamoja na vitabu na broshua za kujifunzia Biblia.

 

 

Ni Nini Kipya

Julai 2023 (Toleo la 14)

  • Tayarisha orodha ya video za kucheza, rekodi za sauti, au picha. Unaweza kupunguza au kuongeza vitu ulivyoweka kwenye orodha hiyo, au kuvicheza kwenye tabo ya Funzo la Kibinafsi.

  • Sasa, jambo lolote unalonakili kwenye maswali ya chapisho la funzo au maelezo ya picha, litatokea katika mfuatano au mpangilio uleule wa habari unayosoma.

  • JW Library kwenye kifaa chako inaweza kutegemezwa na mfumo wa uendeshaji wa Windows 10 Toleo la 1903.

Januari 2023 (Toleo la 13.4)

  • Sera ya Matumizi na Sera ya Faragha zimesasishwa.

  • Mipangilio ya Faragha sasa inakuwezesha kudhibiti taarifa unazotoa kuhusu tovuti na kurasa unazotembelea katika mtandao

Oktoba 2022 (Toleo la 13.3)

  • Sehemu ya kutazama video au ya kusikiliza rekodi za sauti imeongezwa mambo mapya kutia ndani mfumo wa picha ndani ya picha unaokuwezesha kutumia sehemu ndogo tu ya skrini yako kucheza video au kusikiliza rekodi ya sauti huku ukitumia sehemu nyingine za skrini kufanya mambo mengine (ikiwa kifaa chako kina uwezo huo), njia ya kupunguza au kuongeza mwendo wa video au wa rekodi ya sauti inayocheza, na pia ina maandishi yanayojitokeza kwenye video.

  • Unaweza kudhibiti sehemu hizo za kucheza video au rekodi za sauti kwa kutumia ishara. Gusa kwa vidole viwili ili kucheza au kusimamisha video au rekodi ya sauti, telezesha kidole kuelekea kushoto au kulia ili kurudi kwenye video au rekodi ya sauti iliyotangulia au ili kucheza inayofuata, telezesha kidole juu au chini ili kuongeza au kupunguza mwendo, gusa upande wa kushoto au wa kulia mara mbili kwa uharaka ili kurudi nyuma au kusonga mbele.

 

KATIKA SEHEMU HII

Anza Kutumia JW Library​—Windows

Jifunze jinsi ya kutumia sehemu mbalimbali muhimu za JW Library kwenye vifaa vyenye mfumo wa Windows.

Pakua na Utumie Biblia​—Windows

Jifunze jinsi ya kupakua na kutumia Biblia katika JW Library kwenye vifaa vya Windows.

Pakua na Utumie Machapisho​—Windows

Jifunze jinsi ya kupakua na kutumia machapisho kwenye JW Library katika vifaa vya Windows.

Tumia Vialamisho, au, Alama za Kukumbuka Ukurasa​—Windows

Jifunze jinsi ya kutumia alama za kukumbuka ukurasa katika vifaa vyenye mfumo wa JW Library.

Tumia Historia​—Windows

Jifunze jinsi ya kutumia sehemu ya historia kwenye JW Library katika vifaa vyenye mfumo wa Windows.

Panga Habari Kulingana na Mapendezi Yako​—Windows

Jifunze jinsi ya kupanga habari kulingana na mapendezi yako kwenye JW Library katika vifaa vyenye mfumo wa Windows.

Tafuta Katika Biblia au Chapisho​—Windows

Jifunze jinsi ya kutafuta katika Biblia au chapisho, na jinsi ya kutafuta habari kuu kutoka kwenye Insight on the Scriptures katika JW Library katika vifaa vyenye mfumo wa Windows.

Tia Alama Maandishi​—Windows

Jifunze jinsi ya kutia alama maandishi kwenye JW Library katika vifaa vyenye mfumo wa Windows.

Sakinisha JW Library Ikiwa Huwezi Kuipakua Kwenye (App Store) Ukitumia Kifaa cha Windows

Ikiwa huwezi kusakinisha JW Library kwenye kifaa chako cha Windows kutoka kwenye app store rasmi, unaweza kuisakinisha kwa kutumia faili za kusakinisha za JW Library Windows.

Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi​—JW Library (Windows)

Pata majibu ya maswali yanayoulizwa mara nyingi.