Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WATCHTOWER LIBRARY

Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi​—Watchtower Library

Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi​—Watchtower Library

Watchtower Library inatumika kwenye kompyuta ya kawaida au kompyuta ndogo (laptop) inayotumia Microsoft Windows 7 au ya karibuni zaidi. Ikiwa kompyuta yako inatumia ARM processor basi utahitaji kuwa na Microsoft Windows 11.

 

Ukipata ujumbe tena na tena kwamba Watchtower Library imeshindwa kusasisha, fuata hatua hizi ili kusasisha mwenyewe:

  1. Fungua ukurasa wa Sasisha Watchtower Library kwenye jw.org.

  2. Pakua Faili ya Kusasisha Watchtower Library katika lugha yako.

  3. Fuata maagizo chini ya kichwa “Tumia Faili ya Kusasisha.”

Ikiwa bado huwezi kutatua tatizo lako, fuata hatua zifuatazo:

  1. Kwenye File Explorer, fungua folda “C:\ProgramData\Watchtower\WTLibrary.”

  2. Futa faili mbili zifuatazo:

    • a. ca-bundle.zip

    • b. cert.pem

Ikiwa ni vigumu kwako kufuata hatua zilizoonyeshwa hapo juu, mwombe rafiki anayefahamu vizuri Watchtower Library akusaidie, au wasiliana na ofisi yetu ya tawi iliyo karibu.

 

Huenda ukapata msaada kutoka kwa rafiki yako anayefahamu vizuri Watchtower Library. Ikiwa hilo haliwezekani, tafadhali wasiliana na ofisi yetu ya tawi iliyo karibu.