Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

JW LUGHA

Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi​—JW Lugha (iOS)

Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi​—JW Lugha (iOS)

Kithai ni mojawapo ya lugha zenye herufi za kipekee na zenye alama za matamshi. Si mara zote mfumo wa iOS unaandika lugha hizo kwa usahihi.

 

JW Lugha inaweza kutumiwa katika vifaa vifuatavyo:

  • iPhone, iPad, na iPod zenye mfumo wa iOS 12.0 au wa karibuni zaidi)

Utegemezo kwa vifaa vifuatavyo hautapatikana:

  • iPhones, iPad, na iPod zenye mfumo wa iOS 11.0 au zamani zaidi

 

  • Matoleo ya zamani ya JW Lugha yalizima sauti ya programu hiyo mtu alipozima sauti ya mwito kwenye kifaa. Tafadhali sasisha JW Lugha kwenye kifaa chako ili kuhakikisha kwamba una toleo la karibuni zaidi.

  • Angalia ikiwa umezima sauti kwenye kifaa chako. Ikiwa umefanya hivyo, ongeza sauti.

  • Hakikisha kwamba umeongeza sauti kwenye kifaa chako.

 

Katika ukurasa wa mwanzo, bofya sehemu ya Mipangilio kwenye menyu, kisha uchague Mwendo wa Kucheza Rekodi (Global Playback Speed) ili kuongeza au kupunguza mwendo wa sauti.

 

Rekodi ya kusikiliza katika sehemu ya Msamiati inatumia uwezo wa kifaa chako wa kubadili maandishi kuwa rekodi za kusikiliza. Kwa kweli, iOS ina uwezo mdogo wa kubadili maandishi kuwa rekodi za kusikiliza (TTS). Unaweza kupakua programu ya TTS yenye ubora wa juu zaidi. Katika sehemu ya Settings kwenye kifaa chako General > Accessibility > VoiceOver > Speech. Kwa habari zaidi tembelea tovuti hii https://support.apple.com/en-us/HT202362.

 

Lugha kuu ni lugha unayoijua. Unapoanza, chagua Lugha Kuu.

Tazama pia: Ninaweza kubadili lugha kuu jinsi gani?

 

Chagua Mipangilio kwenye menyu kuu, kisha ubadili lugha chini ya Lugha ya Kwanza.

 

Unapopakua Jw Lugha, utaombwa uchague lugha unayotaka kujifunza.

Tazama pia: Ninaweza kubadili lugha ya kwanza jinsi gani?

 

Chagua lugha katika sehemu ya kuchagua lugha.

Ona pia: Je, ninaweza kutumia lugha zaidi ya moja?

 

Ndiyo, unaweza kutumia lugha nyingi wakati uleule. Bofya sehemu ya kuchagua lugha na kisha uchague lugha ya ziada.

Ona pia: Ninaweza kubadili lugha jinsi gani?

 

Bofya menyu karibu na neno, fungu la maneno, au picha, kisha uchague Ongeza kwenye Mkusanyo. Bofya Tengeneza Mkusanyo Mpya ili upange habari jinsi unavyopenda na uipe jina. Unapoongeza mafungu ya maneno ukiwa kwenye Mtandao, habari hizo zinapakuliwa moja kwa moja kwenye kifaa chako ili uzipate bila Intaneti.

 

Bofya menyu kando ya kile unachotaka kunakili au kuondoa. Kisogeze ili upange upya mkusanyo.

 

Ndani ya mkusanyo, bofya Anza Mazoezi ili uone mazoezi yaliyomo:

  • Tazama: Chagua tafsiri ya neno unaloona

  • Patanisha: Chagua maneno yanayofanana na picha, au maneno na tafsiri ya maneno hayo

  • Sikiliza: Sikiliza fungu la maneno na uchague tafsiri sahihi

  • Kadi za Sauti: Fikiria tafsiri ya neno kabla ya kuangalia jibu. Badili mwendo wa kusikiliza unaposikiliza tena. Bofya sehemu ya sauti ili kuchagua kusikiliza tena.

  • Somo la Kusikiliza: Sikiliza maneno yakisomwa kwa sauti.

  • Bofya sehemu ya Hariri ili kusikiliza kwa mfuatano uliochaguliwa au kuchagua mfuatano unaotaka.

 

Ndiyo. Bofya Mipangilio kwenye menyu kuu, kisha utumie sehemu iliyoandikwa Onyesha Maandishi ya Kiroma (Show Romanization) ili kubadili maandishi ya Kiroma.

 

Maandishi yanapatikana muda wote, hata ikiwa hutumii Mtandao. Unapokuwa kwenye Mtandao, bofya fungu la maneno ili kuyasikiliza moja kwa moja. Ili kupakua video na habari za kusikiliza, bofya alama ya kupakua. Ili upakue video na habari zote za kusikiliza katika lugha unayojifunza, kuna maneno Pakua Yote sehemu ya kuchagua lugha, kando ya lugha unayotaka kujifunza.

 

Ndiyo, unaweza kuwa na nakala ya mkusanyo na historia. Katika menyu ya Mipangilio, chagua Hifadhi na Urudishe. Ikiwa tayari unanakili habari zako, unaweza kuzirudisha wakati wowote. Ukirudisha mkusanyo wenye jina sawa na mkusanyo mwingine kwenye kifaa chako, mkusanyo ulio kwenye kifaa utapotea.

 

Unaweza kumwomba rafiki anayejua jinsi ya kutumia programu ya JW Lugha akusaidie. Hilo likishindikana, tafadhali jaza na utume fomu yetu ya msaada mtandaoni