Hamia kwenye habari

Sherehe na Habari Kuhusu Wenyeji wa Asili wa Amerika, New York City

Sherehe na Habari Kuhusu Wenyeji wa Asili wa Amerika, New York City

Watu wengi hufikiri kwamba Wenyeji wa Asili wa Amerika nchini Marekani wanaishi kwenye hifadhi zilizo katika maeneo ya vijijini ya nchi hiyo. Hata hivyo, zaidi ya asilimia 70 ya Wenyeji wa Asili wa Amerika wanaishi mjini. Jiji kubwa kabisa nchini Marekani, New York, lilikuwa na sherehe ya Wenyeji wa Asili wa Amerika inayoitwa “Lango la Mataifa,” pamoja na sherehe ya powwow, kuanzia Juni 5-7, 2015. * Baadhi ya Mashahidi wa Yehova jijini New York walipojua kutakuwa na tukio hilo, mara moja walifanya mipango ili wahudhurie. Kwa nini?

Mashahidi wa Yehova wanatafsiri machapisho yanayotegemea Biblia katika mamia ya lugha, kutia ndani lugha nyingi za Wenyeji wa Asili wa Amerika, kama vile Blackfoot, Dakota, Hopi, Mohawk, Navajo, Odawa, na Plains Cree. Kwa hiyo, Mashahidi walisimamisha meza na vigari vyenye kupendeza kwenye sherehe hiyo na kuonyesha baadhi ya machapisho hayo, kutia ndani trakti You Can Trust the Creator!

Tovuti yetu rasmi pia ina rekodi za kusikiliza na video katika lugha nyingi kati ya hizo. Mashahidi waliohudhuria tukio hilo waliwaonyesha wageni waliopendezwa baadhi ya rekodi hizo. Wageni hao walisema kwamba walitambua kuwa vibanda, mabango, na maonyesho mengine katika sherehe hiyo yalikuwa hasa katika Kiingereza au Kihispania.

Watu wengi waliohudhuria walifurahi kuona kwamba mbali tu na kujitahidi kutafsiri katika lugha nyingi za Wenyeji wa Asili wa Amerika, kazi yetu ya kufundisha Biblia inafanywa kwenye majiji na pia katika hifadhi zao. Baada ya kufahamishwa kuhusu kazi yetu, mfanyakazi mmoja katika tukio hilo aliomba kujifunza Biblia na akasema, “Ninatazamia kwa hamu wakati mtakaponitembelea na kunifundisha kuhusu Biblia!”

Wenzi wa ndoa viziwi ambao ni Wenyeji wa Asili wa Amerika walifika kwenye meza yetu, lakini Mashahidi hawakuweza kuwasiliana nao. Hata hivyo, wakati huohuo Shahidi ambaye amejifunza lugha ya ishara aliwasili. Aliwasiliana na wenzi hao kwa dakika 30 na akawasaidia kujua mahali ambapo kusanyiko la Mashahidi wa Yehova la lugha ya ishara litafanywa karibu na eneo lao.

Mashahidi zaidi ya 50 wa Yehova walishiriki katika jitihada hizo za kufundisha Biblia, na wageni walioongea nao walichukua machapisho zaidi ya 150 katika tukio hilo la siku tatu.

^ fu. 2 Kulingana na William K. Powers, mtaalamu wa tabia na utamaduni, powwow “ni tukio linalohusisha kikundi cha watu wakiimba huku wanaume, wanawake, na watoto wakicheza.”​—Ethnomusicology, Septemba 1968, ukurasa wa 354.