Sijaachwa Peke Yangu
Pakua:
1. Nimesalitiwa na kutelekezwa,
Nimevunjika moyo na
Nimeishiwa na nguvu
Hakuna yeyote anayenijali
Nani anifariji, nani anisaidie?
(KORASI)
Sijaachwa peke yangu
Kwa sababu ninajua
Yehova ananijali
Husikia sala zangu
Na hata iweje, hataniacha.
2. Nitashikamana na Mungu wangu.
Hata nivunjwe moyo, sina wasiwasi nawe
U karibu nami,
Huniachi kamwe.
Nakutumainia,
Hautanitelekeza.
(KORASI)
Sijaachwa peke yangu
Kwa sababu ninajua
Yehova ananijali.
Husikia sala zangu
Na hata iweje, hataniacha
Peke yangu.
Kwa sababu ninajua
Yehova ananijali
Husikia sala zangu;
Na hata iweje,
Hataniacha.