Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 89

Sikiliza, Tii, Upate Baraka

Sikiliza, Tii, Upate Baraka

(Luka 11:28)

  1. 1. Kristo Yesu tukimsikiliza,

    Na kufanya aliyoagiza,

    Tutapata furaha na fanaka,

    Kwa kutii tupate baraka.

    (KORASI)

    Tii ubarikiwe.

    Mungu msikilize.

    Nawe utakuwa na furaha.

    Sikiliza, utii.

  2. 2. Maisha yetu ni kama majengo.

    Kwenye mwamba twaweza kujenga.

    Tumtii Kristo Yesu Kuhani,

    Tuwe na kusudi maishani.

    (KORASI)

    Tii ubarikiwe.

    Mungu msikilize.

    Nawe utakuwa na furaha.

    Sikiliza, utii.

  3. 3. Kama miti kando ya maji mengi,

    Izaavyo matunda kwa wingi.

    Tukitii Mungu kama wanaye,

    Uzima milele hatimaye.

    (KORASI)

    Tii ubarikiwe.

    Mungu msikilize.

    Nawe utakuwa na furaha.

    Sikiliza, utii.