Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Wimbo Na. 26

Mlinitendea Mimi

Mlinitendea Mimi

(Mathayo 25:34-40)

  1. 1. Kondoo wengine, wanatumikia

    Bega kwa bega na ndugu za Kristo.

    Yote yafanywayo

    kwa ajili yao,

    Yesu anasema atawalipa.

    (KORASI)

    “Mkiwafariji, mwanifariji.

    Mlipowatunza, mlinitunza.

    Bidii yenu haikuwa bure.

    Mlipotenda mema yoyote.

    Mlinitendea mema na mimi.”

  2. 2. “Mlinifariji, iwe njaa, kiu.

    Mahitaji yangu, mliandaa.”

    “Bwana tulifanya

    yote hayo lini? ”

    Ndipo Bwana atakapowajibu:

    (KORASI)

    “Mkiwafariji, mwanifariji.

    Mlipowatunza, mlinitunza.

    Bidii yenu haikuwa bure.

    Mlipotenda mema yoyote.

    Mlinitendea mema na mimi.”

  3. 3. “Kwangu mmekuwa, washikamanifu,

    Mnapohubiri na ndugu zangu.”

    Ndipo Kristo Yesu

    atawaambia

    “Urithini uzima wa milele.”

    (KORASI)

    “Mkiwafariji, mwanifariji.

    Mlipowatunza, mlinitunza.

    Bidii yenu haikuwa bure.

    Mlipotenda mema yoyote.

    Mlinitendea mema na mimi.”