Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Koa la Moluska

Koa la Moluska

Je, Ni Kazi ya Ubuni?

Koa la Moluska

Ingawa makoa huonekana dhaifu, kwa kawaida hayawezi kuvunjika kwa urahisi. “Nililazimika kupiga [makoa] fulani kwa nyundo ili niyavunje,” anasema injinia Kenneth Vecchio, akikumbuka siku zake za utotoni. Unaweza kujua kwamba makoa ni magumu unapochunguza koa la moluska. *

Fikira hili: Tabaka la ndani la koa la moluska (linaloitwa lulumizi) lina magamba madogo sana yaliyoachana kidogo sana. “Utata ambao tumeona katika lulumizi ni wenye kustaajabisha sana na ni jambo muhimu ili kufanya kitu kiwe kigumu,” anasema Christine Ortiz, profesa msaidizi wa Idara ya Sayansi na Uinjinia katika Taasisi ya Tekinolojia ya Massachusetts, nchini Marekani.

Mwandishi wa mambo ya kisayansi Charles Petit alifafanua jinsi lulumizi iliyoongezwa ukubwa inavyoonekana kuwa na “utaratibu wa hali ya juu.” Anaeleza: “Ukiangalia kupitia darubini utaona matabaka yaliyopangwa kwa utaratibu ya madini maangavu yenye umbo la pembe sita ya kalisi kaboni yanayoonekana kama matofali yaliyowekelewa moja juu ya lingine. Yanaunganishwa kwa gundi yenye protini nyingi iliyotoka kwa samaki-gamba.”

Wanasayansi wanaamini kwamba muundo wa koa la moluska unaweza kutumiwa kutengeneza vitu vingi kama vile, vitu vigumu zaidi vya kujikinga, mabati ya magari, na mabawa ya ndege, na kadhalika. “Vitu vya asili vina kanuni za muundo zinazoweza kutengeneza vitu vidogo sana ambavyo ni vya hali ya juu,” anasema Ortiz. “Mainjinia hawajafaulu kupata ustadi huo.”

Una maoni gani? Je, koa gumu la moluska lilijitokeza lenyewe? Au je, lilibuniwa?

[Maelezo ya Chini]

^ fu. 3 Moluska ni viumbe wenye miili laini isiyo na mifupa. Moluska wa baharini wanatia ndani chaza, kome, kombe, pweza, na ngisi.

[Picha katika ukurasa wa 25]

Picha iliyoongezwa ukubwa ya tabaka la ndani la koa la moluska

[Hisani]

Inset: © Eye of Science/Photo Researchers, Inc.