Hamia kwenye habari

Mara Nyingi Wagonjwa Ambao Ni Mashahidi Hupona Haraka

Mara Nyingi Wagonjwa Ambao Ni Mashahidi Hupona Haraka

AUSTRALIA: Gazeti The Sydney Morning Herald, la Oktoba 2, 2012 linaripoti hivi: “Wagonjwa ambao ni Mashahidi wa Yehova—ambao hukataa kutiwa damu mishipani kwa sababu za kidini—hupona haraka kuliko wagonjwa wengine.”

Ripoti hiyo inamnukuu Profesa James Isbister kutoka Shule ya Tiba ya Sydney katika Chuo Kikuu cha Sydney. “Profesa Isbister alisema madaktari waliwapatia Mashahidi wa Yehova matibabu bora wakijaribu kuhifadhi damu [ya wagonjwa Mashahidi]. Matokeo ni kwamba walikuwa na uwezekano mkubwa wa kupona, na walikaa hospitalini na katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa muda mfupi zaidi kuliko watu wanaotiwa damu mishipani wakati wa upasuaji,” laripoti gazeti hilo.

Si Daktari Isbister pekee aliye na maoni hayo. Toleo la Julai 2, 2012 la jarida linalotayarishwa na Chama cha Kitiba cha Marekani linasema hivi kuhusu wagonjwa Mashahidi waliofanyiwa upasuaji wa moyo: “Mashahidi hawakupatwa na matatizo mabaya sana yanayotokana na upasuaji na walikaa hospitali kwa muda mfupi wakilinganishwa na wagonjwa ambao walitiwa damu mishipani.”