Hamia kwenye habari

Dada Nataliya Voropaeva

MEI 22, 2023
URUSI

“Woga Hauepukiki Lakini Ujasiri Ni Uchaguzi”

“Woga Hauepukiki Lakini Ujasiri Ni Uchaguzi”

Machi 24, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Zheleznodorozhny iliyoko Krasnoyarsk ilitangaza uamuzi katika kesi inayomhusu Dada Nataliya Voropaeva. Alipigwa faini ya rubo 360,000 (dola 4,730 za Marekani).

Maelezo Mafupi Kumhusu

Kama Nataliya, sisi pia tumeazimia kuwa “hodari na kusema: ‘Yehova ni msaidizi wangu; sitaogopa.’”​—Waebrania 13:6.

Mfuatano wa Matukio

  1. Novemba 2017–Novemba 2020

    Aliwekwa chini ya ulinzi na nyumba yake ilifanyiwa upekuzi. Alihojiwa kama sehemu ya uchunguzi dhidi ya Ndugu Andrey Stupnikov

  2. Septemba 5, 2022

    Kesi ya uhalifu inaanzishwa

  3. Septemba 6, 2022

    Anawekewa vizuizi vya kusafiri

  4. Oktoba 20, 2022

    Anashtakiwa kwa uhalifu

  5. Februari 27, 2023

    Kesi ya uhalifu inaanza

  6. Machi 24, 2023

    Anapigwa faini ya rubo 360,000 (dola 4,730 za Marekani)