Hamia kwenye habari

Kushoto hadi kulia: Dada Tatyana Bondarenko, Dada Tatyana Svoboda, na Dada Yelena Nesterova

JULAI 10, 2023
URUSI

Dada Watatu Wahukumiwa Jijini Komsomolsk-on-Amur

Dada Watatu Wahukumiwa Jijini Komsomolsk-on-Amur

Machi 23, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Centralniy iliyo Komsomolsk-on-Amur iliwahukumu Dada Tatyana Bondarenko, Dada Yelena Nesterova, na Dada Tatyana Svoboda kifungo cha nje cha miaka mitano kila mmoja. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunasali kwamba Yehova aendelee kuwabariki na kuwaimarisha dada zetu wanapodumisha uaminifu chini ya majaribu.​—Ruthu 2:12.

Mfuatano wa Matukio

  1. Septemba 21, 2021

    Kesi ya uhalifu yafunguliwa dhidi ya Tatyana Svoboda

  2. Oktoba 18, 2021

    Maofisa wa polisi waanza pia kuwapeleleza Tatyana Bondarenko na Yelena Nesterova

  3. Oktoba 20, 2021

    Nyumba zao zafanyiwa msako

  4. Agosti 28, 2022

    Mashtaka yafunguliwa

  5. Desemba 28, 2022

    Kesi ya uhalifu yaanza

  6. Machi 23, 2023

    Walihukumiwa kifungo cha nje cha miaka mitano kila mmoja