Hamia kwenye habari

Nyumba iliyoharibiwa nchini Indonesia

APRILI 19, 2021
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE

Indonesia na Timor-Leste Zakumbwa na Kimbunga Seroja

Indonesia na Timor-Leste Zakumbwa na Kimbunga Seroja

Eneo

Visiwa vya East Nusa Tenggara vilivyoko mashariki ya Indonesia na Timor-Leste

Janga

  • Aprili 4, 2021, Kimbunga Seroja kilisababisha uharibifu mkubwa na kuwafanya watu wengi kuhama kutoka makwao

Athari ambazo ndugu na dada zetu wamepata

  • Watu 236 hivi wamelazimika kuhama makazi yao

Uharibifu wa mali

Indonesia

  • Nyumba 45 ziliharibiwa kidogo

  • Nyumba 8 zilipata uharibifu mkubwa

  • Majumba 3 ya Ufalme yalipata uharibifu mdogo

Timor-Leste

  • Nyumba 19 ziliharibiwa kidogo

  • Nyumba 10 zilipata uharibifu mkubwa

Jitihada za kutoa msaada

  • Nchini Indonesia, Halmashauri ya Kutoa Msaada (DRC) iliundwa ili kupanga jinsi msaada utakavyotolewa. Halmashauri hiyo inapanga kazi ya kurekebisha Majumba ya Ufalme yaliyoharibiwa na pia nyumba zilizopata uharibifu mkubwa

  • Waangalizi wa mzunguko katika eneo hilo wanaandaa msaada na faraja ya kiroho kwa ajili ya wahubiri walioathiriwa

  • Mara tu baada ya kimbunga hicho, wazee wa makutaniko walitafuta mahali pa kulala pa muda kwa ajili ya ndugu na dada waliolazimika kuhama makazi yao. Pia wazee walisambaza chakula, maji, na mahitaji mengine ya lazima. Pia walisaidia kupanga kazi ya kusafisha nyumba zilizoharibiwa

  • Huko Timor-Leste, wazee wameanza kazi ya kusafisha nyumba zilizoharibiwa na kusambaza chakula na mahitaji mengine kwa ajili ya wale wenye uhitaji. Pia, wazee wamepanga makazi ya muda kwa ajili ya wale waliolazimika kuhama

  • Jitihada zote za kutoa msaada zinafanywa kupatana na sheria za usalama za COVID-19

Tunashukuru kwa ajili ya msaada ambao Yehova anaandaa kupitia “huduma . . . ya kutoa msaada” ya kutaniko la Kikristo.—2 Wakorintho 9:13.