Hamia kwenye habari

Nyumba zilizokumbwa na mafuriko katika Jimbo la Rivers, Nigeria

NOVEMBA 13, 2020
NIGERIA

Mafuriko Yasababisha Vifo Nchini Nigeria

Mafuriko Yasababisha Vifo Nchini Nigeria

Mvua kubwa zilizonyesha kati ya Septemba na Oktoba 2020 zilisababisha mafuriko makubwa katika majimbo mengi nchini Nigeria. Mafuriko hayo yameharibu vibaya sana mashamba na majengo mengi. Inasikitisha kwamba ndugu yetu mmoja alikufa kwa sababu ya janga hilo. Kwa kuongezea, zaidi ya wahubiri 1, 828 walilazimika kuhama nyumba zao na nyumba za ndugu wengine 62 zimeharibiwa.

Ofisi ya tawi ya Nigeria imeweka rasmi Halmashauri 7 za Kutoa Msaada ili kuratibu kazi ya kutoa msaada na wakati huohuo wakitii miongozo ya kujilinda dhidi ya COVID-19. Waangalizi wa mzunguko na wazee wa makutaniko wanashirikiana kwa ukaribu ili kuwasaidia akina ndugu na dada walioathiriwa kimwili na kiroho.

Jumba la Ufalme lililokumbwa na mafuriko katika Jimbo la Delta, Nigeria

Tunasikitika kwamba mafuriko hayo yamesababisha vifo. Tunajua kwamba Yehova, Mungu wa wokovu wetu, ataendelea kuwafariji na kuwategemeza ndugu zetu katika kipindi hiki kigumu.—Zaburi 68:19.