Hamia kwenye habari

JUNI 24, 2019
EKUADO

Guayaquil, Ekuado—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe”

Guayaquil, Ekuado—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe”
  • Tarehe: Juni 14-16, 2019

  • Mahali: Estadio Monumental Banco Pichincha iliyopo Guayaquil, Ekuado

  • Lugha ya Programu: Lugha ya Ishara ya Ekuado, Kiingereza, Kihispania

  • Idadi ya Wahudhuriaji: 53,055

  • Idadi ya Waliobatizwa: 702

  • Idadi wa Wajumbe Kutoka Mataifa Mbalimbali: 5,300

  • Ofisi za Tawi Zilizoalikwa: Argentina, Ubelgiji, Bolivia, Amerika ya Kati, Kolombia, Kuba, Kazakhstan, Korea, Moldova, Myanmar, Poland, Hispania, Marekani

  • Mambo Yaliyoonwa: José Francisco Cevallos, rais wa Klabu ya Michezo ya Barcelona inayomiliki uwanja huo wa michezo, alisema hivi: “Hatujawahi kupata malalamiko yoyote kuhusiana na makusanyiko yenu, si hili tu hata makusanyiko mengine yaliyowahi kufanyika hapa. Jambo hilo linaonyesha jinsi mlivyo na mwenendo mzuri na mpangilio, ni mambo tunayoyaona katika makusanyiko yenu yote. Hilo si jambo rahisi, lakini hiyo ndiyo desturi yenu, kupangilia mambo kikamili kwa ajili ya matukio yenu yote. Nyinyi ni watu wazuri—walioelimika, wenye mwenendo mzuri, na mnapangilia mambo vizuri. Tunapendekeza Mashahidi wa Yehova wakaribishwe katika jiji lolote au nchi yoyote.”

 

Wajumbe wakipiga picha wakiwa Betheli ya Ekuado katika siku ya wageni

Ndugu na dada wenyeji wakiwa pamoja na wajumbe utumishi

Wajumbe kutoka mataifa mbalimbali wakiimba kwa pamoja katika siku ya kwanza ya kusanyiko

Baadhi ya ndugu na dada 702 wapya wakiwa wanabatizwa

Wajumbe wakiandika mambo makuu ya sehemu inayoendelea

Wajumbe wakionyesha ishara ya upendo ya Kikorea

Ndugu Kenneth Cook, mshiriki wa Baraza Linaloongoza, akitoa hotuba ya mwisho kusanyikoni siku ya Jumapili

Watumishi wa wakati wote wakiwapungia watu mkono katika siku ya mwisho ya kusanyiko

Ndugu na dada wenyeji wakicheza dansi ya kitamaduni katika pindi ya burudani jioni moja