Hamia kwenye habari

Jengo lililoanguka kwenye mji wa Antakya, Uturuki

FEBRUARI 10, 2023 | HABARI ZILIONGEZWA: FEBRUARI 17, 2023
Uturuki

HABARI ZA KARIBUNI—Makumi ya Maelfu Waathiriwa na Tetemeko Kubwa Uturuki

HABARI ZA KARIBUNI—Makumi ya Maelfu Waathiriwa na Tetemeko Kubwa Uturuki

Asubuhi ya Jumatatu, Februari 6, 2023, tetemeko la ardhi lenye kipimo cha 7.8 lilitokea upande wa kusini magharibi wa Uturuki. Baadaye tetemeko lingine lenye kipimo cha 7.5 lilitokea katika eneo hilo. Isitoshe, kumekuwa na matetemeko mengine madogo-madogo pia. Zaidi ya watu 38,000 wamekufa na zaidi ya watu 108,000 wamejeruhiwa.

Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata Nchini Uturuki

  • Inasikitisha kwamba dada 1 mwenye umri mkubwa alikufa katika jiji la Adana. Isitoshe, ndugu mmoja, mke wake, na watoto wao wawili wadogo walikufa katika jiji la Adiyaman

  • Nyumba 3 ziliharibiwa kabisa

  • Nyumba 17 zilipata uharibifu mkubwa

  • Nyumba 22 zilipata uharibifu mdogo

  • Jumba 1 la Ufalme limepata uharibifu mkubwa

  • Majumba 2 ya Ufalme yamepata uharibifu mdogo

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Akina ndugu wanaoongoza wanawafariji wale ambao wameathiriwa na msiba huo kwa kuwapa msaada wa kiroho unaohitajika

  • Halmashauri 2 za Kutoa Msaada zimeanzishwa ili kusimamia jitihada za kutoa msaada

Mshiriki wa Halmashauri ya Tawi akiwafariji kwa Maandiko baadhi ya ndugu na dada zetu ambao nyumba zao zilipata uharibifu mkubwa au kuharibiwa kabisa

Licha ya matetemeko hayo yenye kutisha, ndugu zetu wanapata faraja kwa sababu wanajua kwamba Yehova “ni kimbilio letu na nguvu zetu, msaada unaopatikana kwa urahisi nyakati za taabu.”​—Zaburi 46:1.